top of page
Search

Thamani.

  • Writer: kevinmoishyleez
    kevinmoishyleez
  • Jul 18, 2021
  • 1 min read

Baba kabla hajafa alimwambia mwanae "hapa nina saa niliyopewa na babu yako ina miaka zaidi ya mia mbili,nataka nikuzawadie.Lakini kabla sijakupa nenda kwa sonara uone kama watainunua kwa shilingi ngapi?" Kijana akaenda na kumrudia babaake na kumwambia kuwa wamesema watainunua kwa shilingi elfu kumi na tano kwa sababu imezeeka sana. Babaake akamwambia tena aende kwenye maduka ya vyuma chakavu,Alipoenda aliambiwa kuwa watainunua kwa shilingi elfu moja. Baada ya hapo baba alimwambia aende tena kwenye jumba la makumbusho aone watainunua kwa shilingi ngapi. Alipoenda wao wakamwambia watainunua kwa shilingi milioni kumi na tano,kwa sababu walikuwa wanatafuta sana vitu vya kale kama hivyo. Baada ya hapo baba alimwambia mwanae nilitaka tu ujue thamani ya kitu kikiwa sehemu yake sahihi. "Mwanangu unaweza ukaenda mahali watu wasikupe hashima yako na wasikuthamini kabisa. Usije umia kwa sababu hawajui thamani yako ukiona hivyo!Toka mahala hapo tambua hapo sio mahali sahihi kwako tafuta mahali pengine sahihi ambapo watatambua thamani yako...."



 
 
 

Recent Posts

See All
Friday motivation

You Don’t Have To Be Great To Start, But You Have To Start To Be Great. Dont limit Your Challengers. Challenge Your Limits.

 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

+254703970958

©2021 by Kevin Moishyleez. Proudly created with Wix.com

bottom of page